IGP Sirro awatoa hofu wananchi tishio la ugaidi Tanzania

IGP Simon Sirro amezungumzia taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania iliyotoa tahadhari ya kutokea kwa ugaidi katika hoteli za Masaki na maduka ya Slipway, Msasani Peninsula Jiji la Dar es Salaam akiwataka wananchi kutokuwa na hofu.

IGP Sirro amesema, “hiyo ni taarifa kama taarifa nyingine, inaweza kuwa ya kweli au uongo, lakini sisi kama vyombo vya ulinzi huwa hatupuuzi jambo. Tangu jana (Jumanne Juni 17, 2019) tulipata hiyo taarifa kwa hiyo tuko vizuri, timu zetu za operesheni na intelijensia na wengine tunaifanyia kazi.”

 

Related Posts