WAJUMBE KUTOKA NCHI 12 WA SHIRIKISHO LA WAKUU WA POLISI WA NCHI ZA MASHARIKI MWA AFRIKA (EAPCCO) WAMETEMBELEA SHULE YA POLISI MOSHI (TPS) KWA AJILI YA KUJIFUNZA NA KUONA MAFUNZO YANAYOTOLEWA NA SHULE HIYO. SHIRIKISHO HILO LINAENDELEA NA MKUTANO MKUU AMBAO KESHO SEPTEMBA 20 NI SIKU YA MKUTANO WA WAKUU WA POLISI WA NCHI WANACHAMA.

Askari wa mafunzo ya uongozi mdogo, katika Shule ya Polisi Moshi (TPS) wakiwa katika mafunzo ya mbinu za ulengaji shabaha (pivot drill). Shule ya Polisi Moshi ilitembelewa na baadhi ya Wajumbe nchi 12 wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika EAPCCO kwa ajili ya kuona mafunzo yanayotolewa na Shule hiyo. Picha na Jeshi la Polisi.

Askari wa Kikosi cha Mbwa na Farasi cha Shule ya Polisi Moshi (TPS) wakiwa katika mwendo wa kasi(mwendo wa dharura) wakati wa onesho la miendo mbalimblai ya farasi walipotembelewa na baadhi ya wajumbe kutoka nchi 12 za Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi xza Mashariki mwa Afrika kwa ajili ya kujifunza na kuona mafunzo yanayotolewa na Shule ya Polisi Moshi (TPS). Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi (TPS), KAMISHNA Msaidizi Mwandamizi, Ramadhani Mungi akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa Nchi za Mashariki mwa Afrika walipotembelea Shuleni hapo kwa ajili ya kuona mafunzo mbalimbali ya kijeshi yanayofundishwa hapo. Picha na Jeshi la Polisi.

Related Posts