POLISI KATAVI YAKAMATA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZA SILAHA

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Katavi limemkamata mtu mmoja anayefahamika kwa jina Emmanuel Mahanga maarufu kwa jina la Rambo miaka 56 muhutu mzaliwa wa nchi ya Burundi mkazi wa kijiji cha Busongola Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi akiwa anamiliki mtambo mmoja wa kutengeneza silaha haramu aina ya gobore na risasi zake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Benjamin E. Kuzaga – ACP alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 04.3.2020 majira ya jioni Kijijini kwake Busongola.

 

Related Posts