IGP SIRRO AONGOZA KIKAO CHA UTENDAJI 02/12/2020 DODOMA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiongoza kikao cha Utendaji kazi cha Maofisa Wakuu wa Makao Makuu ya Polisi jijini Dodoma leo 02/12/2020, kujadili utendaji wa kazi za Jeshi hilo, kufanya tathmini ya mafanikio, changamoto kwa kipindi kilichopita na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi kwa ufanisi zaidi katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
Kushoto kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Dkt. Mussa A. Mussa, Kamishna wa Intelijensia CP Charles Mkumbo na Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi DCP Ruta na kutoka kulia kwa IGP Sirro ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai CP Robert Boaz, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas akifuatiwa na Kaimu Kamishna wa Fedha na Lojistiki DCP Lucas Mkondya.

Related Posts