WATENDAJI WA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI.

SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA 2020.

Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto lililopo chini ya usimamizi wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii inayoongozwa na CP, Dkt Mussa Ali Mussa lilifanya maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kitaifa katika Mkoa wa Mjini  Magharib visiwani Zanzibar.

Jeshi la Polisi liliandaa shughuli mbalimbali ikiwemo mandamano yaliyohusisha majeshi mbalimbali pamoja na wanafunzi kutoka katika baadhi ya shule za msingi na sekondari  za visiwani humo ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikua ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh Tabia Maulid Mwita.

Katika maadhimisho hayo watendaji wa Dawati la Jinsia kutoka katika mikoa yote Tanzania bara na Visiwani walishiriki maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kufanya Mkutano wao wa Mwaka kwa siku mbili wa kujitathmini mafanikio na changamoto.

Baada ya Mkutano huo Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto wakiongozwa na Kamishna wa Ushirikihswaji wa Jamii Dkt. Mussa Ali Mussa waliandaa ziara za kutembelea vituo vya kulelea wazee wasiojiweza vya Welezo na Sebuleni Visiwani Unguja.

Katika ziara hiyo ya vituo vya kulea wazee, Jeshi la Polisi lilipata fursa ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo nguo, sabuni, viatu, mafuta, magodoro ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo hayo na kupanda miti. Baada ya shughuli hizo watendaji hao walipata pia fursa ya kula chaku la cha pamoja na wazee wanaotunzwa katika vituo hivyo.

Watendaji wa Dawati pia walipata fursa ya kufanya Utalii wa Ndani kwa kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Visiwani humo ili wawe mabalozi kwa watanzania wengine katika kuutangaza utalii wa ndani.

Baada ya ratiba ya shughuli za watendaji wa Dawati Visiwani unguja kumalizika, watendaji wote wa Dawati wakiongozwa na Mkuu wa Dawati wa Jinsia na Watoto, Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Maria Nzuki waliekea Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya ufunguzi wa Madawati ya Jinsia na Watoto ya Wilaya za Bahi na Kondoa mkoani Dodoma ambapo ufunguzi wa Madawati hayo wageni rasmi walikua ni Wakuu wa Wilaya wa Wilaya hizo.  

Related Posts