Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda, Kamishna Jenerali Dan Munyuza

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda, Kamishna Jenerali Dan Munyuza, alipofanya ziara ya kikazi nchini Tanzania tarehe 10/05/2021 ambapo Wakuu hao pia walifanya kikao cha pamoja katika Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam na kukubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala ya kiusalama ikiwemo udhibiti wa makosa ya uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa binadamu na biashara ya dawa za kulevya.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi zawadi mgeni wake ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda, Kamishna Jenerali Dan Munyuza (kulia), wakati alipofanya ziara ya kikazi nchini Tanzania tarehe 10/05/2021, ziara ya IGP wa Rwanda ililenga kuendelea kukuza na kudumisha ushirikiano katika masuala ya kiusalama ikiwemo udhibiti wa makosa ya uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa binadamu na biashara ya dawa za kulevya.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa kwenye Picha ya pamoja na mgeni wake ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda, Kamishna Jenerali Dan Munyuza, wakati alipofanya ziara ya kikazi nchini Tanzania.

Related Posts