JAMII YATAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI-12/08/2021 ZANZIBAR

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameitaka jamii kujiepusha na kuacha vitendo vya udhalilishaji na biashara ya dawa za kulevya kwani vyombo vya dola vitatumia sheria zilizopo kuwashughulikia wanaojihusisha na vitendo hivyo.

IGP Sirro alisema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa Cheo cha Sajenti wa Polisi yaliyofanyika kwa muda wa miezi miwili katika Chuo cha Polisi Zanzibar ambapo jumla ya wahitimu 1297 walihitimu mafunzo hayo na kupandishwa vyeo.

Hata hivyo, IGP Sirro aliwataka askari hao waliohitimu kutumia mafunzo hayo kuongeza weledi na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi sambamba na kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia.

Katika mafunzo hayo, wapo baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye usahihi wa vitendo na kusikiliza maelekezo wanayopewa na wakufunzi wao ambapo jumla ya wanafunzi kumi walitunukiwa cheti cha mwanafunzi bora na waliofanya vizuri.

Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mafunzo hayo

Related Posts