MAOFISA 20 WA TAWA WAHITIMU MAFUNZO YA AWALI YA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI.

Mkuu wa Chuo Cha Polisi Kidatu, ACP Zarau Mpangule tarehe 03/09/2021 alifunga rasmi mafunzo ya awali ya upepelezi wa Makosa ya Jinai kwa Maofisa 20 wa TAWA yaliyofanyika kwenye Chuo.

Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleleza Makosa ya Jinai kwa kesi za wanyamapori na misitu Maofisa wa TAWA yalianza mnamo tarehe 07/07/2021 katika Chuo Cha Maofisa wa Polisi Kidatu Mkoani Morogoro.

Akizungumza katika ghafla hiyo ACP Mpangule alisema ” lengo la mafunzo haya ni kuwapa ujuzi, stadi, utayari na uwezo zaidi wa kufanya kazi kwa weledi wakati wa kutekeleza majukukumu yenu kwa kuzingatia misingi ya sheria za nchi na utawala bora, hivyo mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwani serikali inatilia mkazo ulinzi wa rasilimali zetu hasa wanyamapori”

Nae Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi Bw. Sylvester Mushi akimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA alisema “Jeshi la Uhifadhi limepata Mamlaka ya kupeleleza makosa yote ya jinai yanayohusu uhalifu dhidi ya rasilimali za wanyamapori na misitu chini ya kifungu Cha 104 (2) Cha sheria ya mabadiliko ya sheria mbalimbali Namba 2 ya Mwaka 2020 kikisomeka na kifungu Cha 4(2) Cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai namba 20 Kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2019 hivyo ili kutekeleza jukumu hilo la kupeleleza  Jeshi linahitaji kuwajengea uwezo maafisa wake ili waweze kutekeleza majukukumu Yao kwa ufanisi na weledi”.

Related Posts