RPC Kilimanjaro

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limeendelea na Operesheni maalum ya kupambana na dawa za kulevya na kufanikiwa kukamata Bangi misokoto 3075 sawa na Kg 5, Pombe ya Moshi Lita 105, Mirungi Kilo 241, Gari moja aina ya Grand Mark II na Pikipiki 4 ambazo zilitumika kusafirisha dawa za kulevya.
Kufuatia Operesheni hiyo maalum pia jumla ya watuhumiwa 40 wamekamatwa kwa makosa ya kujihusisha na uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.

katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 kwa makosa ya mauaji yaliyotendeka katika vipindi tofauti tofauti na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika

Related Posts