Mkuu wa Mkoa wa Pwani afungua mashindano ya mpira wa miguu kombe la UHALIFU HAULIPI CUP

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge, leo Septemba 28, 2021 amezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wa halmashauri ya Mji wa Kibaha.
Mashindano yenye lengo la kuwaleta pamoja vijana na Jeshi la Polisi juu ya mapambano ya uhalifu na wahalifu

Mashindano hayo yamepewa jina la UHALIFU HAULIPI CUP yaliyoanzishwa na Jeshi la Polisi chini ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa – ACP, ambapo jumla ya timu 16 zitashiriki kwenye mashindano hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku 16 na Bingwa wa mashindano hayo atapata Ng’ombe mmoja na pesa taslimu kiasi cha Tsh 100,000/= pamoja na zawadi nyingine

Hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Chama cha Mpira wa Miguu Kibaha (Kibafa) wananchi na wageni wengine waalikwa

Related Posts