IGP Sirro akutana na baadhi ya Viongozi wa Makampuni binafsi ya ulinzi

Matukio mbalimbali Pichani yakimuonyesha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro alipokutana na baadhi ya Viongozi wa  Makampuni binafsi ya Ulinzi Makao Makuu ya Polisi jijini Dodoma Septemba 29, 2021 ambapo katika kikao hicho pia walihudhuria Makamishna wa Polisi wa Makao Makuu na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kukuza ushirikiano kwani wote wanajenga nyumba moja.Aidha, IGP Sirro alitoa maelekezo baada ya kukubaliana kwenda kuyafanyia kazi ili kuondoa changamoto zilizopo ili Makampuni yote yaweze kuwa kitu kimoja katika kutekeleza majukumu yao na kurahisisha usimamizi

Related Posts