KUTOKA KILIMANJARO CHUI AVAMIA ZAHANATI NA KUJERUHI WANNE

WATU wanne wamejeruhiwa na Chui anayedhaniwa kutoka hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) na baadaye kuvamia zahanati ya Huruma wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.
Hata hivyo Mnyama huyo alidhibitiwa kwa ushirikiano baina ya askari wa wanyapori (TAWA), hifadhi ya mlima Kilimanjaro pamoja na Jeshi la Polisi kabla ya kuleta madhara zaidi kwa wananchi

Majeruhi katika tukio hilo ni Emmanuel Usara (37), Jesca Nnko(21),Urusula Cosmas (26) na Maliki Sakia(31) wote wakazi wa Bomang’ombe wilaya ya Hai.
 Majeruhi wanaendelea vyema katika hospitali ya wilaya ya Hai wakiwa Chini ya uangalizi wa madaktari ili pia kufanyiwa uchunguzi iwapo Mnyama huyo ana magonjwa ya kuambukiza.
Wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika Jeshi la Polisi pamoja na Mamlaka nyingine iwapo wataona wanyama Katika Makazi yao.
Kwa upande wake mganga mkuu wa hospital ya Wilaya ya Hai, Dkt Irene  alithibitisha kupokea majeruhi wa tukio Hilo na kuongeza Kwamba uchunguzi wa kitaalamu unafanyika.Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amethibitisha kitokea kwa tukio hilo.

Related Posts