JESHI LA POLISI MKOA WA RUKWA LAENDELEZA MIKAKATI KUDHIBITI AJALI ZA BARABARANI

Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa tarehe 29.09.2021 limefanya ukaguzi wa mabasi yanayofanya safari katika Mkoa huo pamoja na  kutoa elimu kwa madereva na abiria ambapo zaidi ya mabasi 60 yalikaguliwa kisha kuruhusiwa kuendelea na safari.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Rukwa Mrakibu wa Polisi Gumha amesema licha ya elimu kutolewa kwa madereva pia takribani  abiria 700 walipatiwa elimu ya usalama barabarani na umuhimu wa kufunga mikanda wakati wakiwa kwenye vyombo vya usafiri.

Amewasihi  abiria kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi endapo wataona vitendo vya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani vinavyofanywa na baadhi ya madereva ambavyo vinaweza kusababisha ajali na kupelekea vifo na majeruhi.

Kufuatia ukaguzi huo baadhi ya magari yaliyokuwa na mapungufu mbalimbali yalizuiliwa kuendelea na safari na  mengine yalitozwa faini kulingana na makosa ya magari hayo.

Kamanda Gumha amesema zoezi hilo litakuwa endelevu ili kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa, lakini pia elimu itaendelea kutolewa kwa abiria ili tuweze kuondokana na ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva ama abiria kushabikia mwendo kasi.

Related Posts