IGP SIRRO AKABIDHI UNYEKITI EAPCCO

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amekabidhi rasmi uwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika EAPCCO na kumkabidhi uwenyekiti huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Congo IGP Dieudonne Bahigwa.
Hafla ya kukabidhi unyekiti huo imefanyika Oktoba 14, 2021 nchini Congo ambapo jumla ya nchi 14 wanachama wa shirikisho hilo wamehudhuria hafla hiyo ya makabidhiano. IGP Sirro ameliongoza Shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo ambapo wakati wa uongozi wake amesaidia shirikisho hilo katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa dawa za kulevya, ugaidi pamoja na matishio mengine ya kiusalama.Aidha, kufuatia ushirikiano wa wakuu hao wa Polisi kumewezesha kufanyika kwa operesheni za pamoja sambamba na ubadilishanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Related Posts