KITUO CHA POLISI MBANDE WILAYANI KONGWA CHAZINDULIWA SIKU YA KUMBUKUMBU YA NYERERE

Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamiiwa Jeshi la Polisi DktMussaA.Mussa amezindua rasmi kituo cha Polisi Mbande kilichopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma, kituo hicho chenye hadhi ya daraja C kimejengwa kufuatia maombi ya wananchi wa eneo hilo kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano, Hayati Dkt John Magufuli alipopita katika eneo hilo ambapo wananchi walimweleza kuwa, wanachangamoto ya kituo cha Polisi kutokana na vitendo vya kiuhalifu kwenye eneo hilo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Onesmo Lianga amesema kuwa hali ya uhalifu kwa mkoa wa Dodoma imeendelea kuimarika na kwamba kukamilika kwa kituo hicho kutasaidia kupunguza matukio ya uhalifu na kuwataka wananchi kukitumia kituo hicho kama sehemu rahisi ya kutolea taarifa za uhalifu na wahalifu 

Kituo cha Polisi Mbande kimejengwa kutokana na ushirikiano wa wananchi na wadau wengine wa maendeleo ambapo Hayati Dkt. Magufuli alichangia kiasi cha shilingi milioni tano.

Related Posts