JESHI LA POLISI KUKABILIANA NA MAKOSA YA UDHALILISHAJI NA UKATILI WA KIJINSIA

Jeshi la Polisi nchini limeelezea uwepo wa makosa ya udhalilishaji kwenye jamii na
likitaja kupungua kwa vitendo hivyo katika baadhi ya maeneo huku maeneo
mengine udhalilishaji ukitajwa kuongezeka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Kamishna wa Kamisheni ya
Ushirikishwaji wa Jamii CP Dkt. Mussa A. Musssa wakati akifungua mkutano wa
tatu wa Makamishna na Makamanda wa Polisi wa Mikoa Tanzania katika
kuimarisha upatikanaji wa haki jinai kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.
Aidha,Dkt. Mussa, amesisitiza kuwa, Jeshi la Polisi litaendelea kujikita katika
kuandaa mipango mbalimbali ili kutatua changamoto walizonazo wananchi
ikiwemo makosa yanayotokana na ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto bwana Koshuma Mtengeti amesema kuwa, kwa muda wa miaka kumi sasa wamekuwa wakishirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha wanashughulikia kesi za ukatili wa kingono na makosa mengine dhidi ya watoto.

Related Posts