POLISI KUTUMIA TEHAMA KUTATUA CHANGAMOTO

Na. A/INSP Frank Lukwaro- Jeshi la Polisi.

Watendaji ndani ya Jeshi la Polisi wametakiwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kazi zao za kila siku ili waweze kutoa huduma bora kwa wateja ambao ni Wananchi wanaotumia huduma za kipolisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Fedha na Lojistiki Hamad Hamis Hamad wakati akifunga  mkutano wa siku nne kwa Maafisa Wanandhimu, Wakuu wa Usalama barabarani na Wahasibu wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar uliokuwa ukifanyika Shule ya Polisi Tanzania- Moshi, Mkoani Kilimanjaro ulikuwa na lengo la kuboresha utendaji kazi kwa washiriki hao pamoja na kujiimarisha katika utumiaji mifumo ya kidigitali katika kukusanya mapato ya serikali ikiwemo tozo za barabarani.

Kamishna Hamad amesema Serikali kwa sasa imejikita katika matumizi ya TEHAMA na Jeshi la Polisi kama taasisi ya Serikali ni muhimu kwa watendaji wake kujikita katika kuitambua na kuitumia.

“Mifumo hii ni muhimu na Kitengo chetu cha TEHAMA watusaidie katika kuhakikisha kuwa hatuachwi nyuma katika kutoa huduma zetu kwa kuunganisha mifumo yetu na taasisi nyingine za Serikali ambazo tunafanyanazo kazi hususani katika kukusanya mapato ya Serikali” Alisema Hamad

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Fulgence Ngonyani amesema mkutano huo umewawezesha washiriki kujua jinsi ya kutumia mashine mpya za ukusanyaji wa mapato (POS) ambazo zimenunuliwa na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuboresha ukusanyaji mapato.

DCP Ngonyani alisema wameweka maazimio ambayo kila mmoja anatakiwa kwenda kuyatekeleza ili kuleta tija na kuondoa baadhi ya mapungufu na hoja ambazo zimekuwa zikijitokeza hususani katika udhibiti wa vielelezo vinavyohifandiwa katik vituo vya Polisi.

Mkutano huo pia ulishirikisha wadau wa nje wakiwemo Wizara ya Fedha na Mipango, Mamlaka ya udhibiti wa Ardhini (LATRA), Ofisi ya Mhakiki mali wa Serikali ambapo wameweza kuwasilisha mada zao na kufanya majadiliano ya pamoja ili kuboresha ushirikiano uliopo baina ya taasisi hizo na Serikali.

Kamishna wa Fedha na Lojistiki Hamad Hamis Hamad akizungumza wakati wa  ufungaji wa Mkutano wa Maafisa Wanadhimu wa mikoa, Wakuu wa Usalama barabarani wa mikoa na Wahasibu wa Polisi uliokuwa ukifanyika Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kutathmini mfumo wa ukusanyaji mapato ya Serikali kwa njia ya mtandao. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi

Maafisa Wanadhimu wa mikoa, Wakuu wa Usalama barabarani wa mikoa na Wahasibu wa Polisi wakisikiliza mada mbalimbali katika mkutano wao uliokuwa ukifanyika Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kutathmini mfumo wa ukusanyaji mapato ya Serikali kwa njia ya mtandao. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)

Maafisa Wanadhimu wa mikoa, Wakuu wa Usalama barabarani wa mikoa na Wahasibu wa Polisi wakisikiliza mada mbalimbali katika mkutano wao uliokuwa ukifanyika Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kutathmini mfumo wa ukusanyaji mapato ya Serikali kwa njia ya mtandao. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)

Meneja Mkuu wa Ushirika wa kuweka na kukopa wa Polisi (URA SACCOS) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kim Mwemfula akitoa mada katika Mkutano wa Maafisa Wanadhimu wa mikoa, Wakuu wa Usalama barabarani wa mikoa na Wahasibu wa Polisi uliokuwa ukifanyika Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kutathmini mfumo wa ukusanyaji mapato ya Serikali kwa njia ya mtandao. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi

Related Posts