KAMISHNA WAKULYAMBA AMEZUNGUMZA NA MAAFISA, WAKAGUZI NA ASKARI TOKA JIJINI DODOMA.

Mwenyekiti wa Ushirika wa Chama cha kukopa na kuweka Akiba, Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, CP BENEDICT WAKULIYAMBA leo tarehe 21/12/1021 ametoa wito kwa Maafisa, Wakaguzi za Askari Polisi wa Makao Makuu na Askari wa Jiji la Dodoma na aliwataka wanachama  wa mfuko huo wa kuweka na kukopa wa Jeshi la Polisi (URA SACCOS)  kuhakisha wanongeza Akiba zao na kununua hisa za kutosha ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika ukumbi wa Polisi Jamii uliopo mkoani Dodoma  CP Wakulyamba amesema Chama cha Kuweka Akiba na Kukopa URA SACCOS  kina wanachama wapatao zaidi ya 42.000 pamoja na matawi 7 nchini, huku akiwataka maafisa na askari ambao bado hawajajiunga waweze kujiunga kwasababu ni  mfuko ambao una riba ndogo kuliko mifuko yoyote ya kuweka na kukopa.

Related Posts