IGP Sirro afunga mafunzo ya Koplo

Leo Disemba 23, 2021Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amehitimisha rasmi Kozi ya Uongozi Mdogo Ngazi ya Cheo cha Koplo wa Polisi ambapo jumla ya askari 1697 wamehitimu na kutunukiwa cheo hicho cha Koplo.
IGP Sirro ameendelea kuwakumbusha askari wahitimu, juu ya wajibu wao katika kuhakikisha wanatenda haki, kuwa na lugha nzuri kwa mteja sambamba na kuzingatia sheria, kanuni na  taratibu za nchi.
Aidha, IGP Sirro amewataka askari wahitimu na wale wanaokwenda kufanya kazi za usalama barabarani kuhakikisha wanatoa elimu kwa watu wanaowahudumia.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi SACP Ramadhani Mungi, amesema kuwa, shule hiyo iliwapokea jumla ya wanafunzi 1712 na waliofanikiwa kuhitimu ni 1697 huku 15 wakiachishwa mafunzo kutokana na sababu mbalimbali.

Related Posts