Nidhamu Haki Weledi na Uadilifu ni msingi wa mafanikio Yetu.

WhatsApp Image 2024-01-31 at 3.31.02 PM

Askari 32 watunukiwa vyeti vya pongezi Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Filemon Makungu ametoa vyeti vya pongezi kwa askari 32 waliofanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo kwa mwaka 2023.

Vyeti hivyo vimetolewa Januari 27,2024 wakati wa maadhimisho ya siku ya familia ya Polisi yaliyofanyika mkoani humo yakiambatana na paredi na maonesho ya michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku,kuvuta kamba,mbio za magunia na mpira wa miguu.

Kamanda Makungu amesema lengo la kutoa vyeti hivyo vya pongezi ni kutambua kazi wanazozifanya askari na kuongeza morali ya utendaji kazi.

Pamoja na hayo ACP Makungu amewataka askari wa Mkoa wa Kigoma kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii

Related news