Nidhamu Haki Weledi na Uadilifu ni msingi wa mafanikio Yetu.

c1

CP Dkt Mussa aagwa Rasmi baada ya kumaliza Utumishi wake Jeshini.

Jeshi la Polisi Nchini limemuaga rasmi aliyekuwa kamishna wa Kamisheni ya ushirikishwaji Jamii ambaye kwa sasa ni Katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro kamishna wa Jeshi la Polisi mstaafu CP Dkt Alhaji Mussa Ali Mussa Baada ya kumaliza muda wake wa utumishi ndani ya Jeshi la Polisi.

Akiongea mara baada ya Gwaride maalumu la kumuaga Kamishna mstaafu CP Dkt. Mussa Ali Mussa amesema alijiunga na Jeshi hilo mwaka 1989 Baada ya kumaliza elimu yake ya juu kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam 1988 akiwa ni kijana wa kwanza kutoka Zanzibar akiwa na shahada ya Masomo ya Kiswahili na historia ambapo alijiunga na Jeshi hilo.

Dkt. Mussa ameongeza kuwa katika utumishi wake amehudumu na kushika nafasi tofauti katika maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar ambapo amebainisha kuwa anamshukuru Mungu kwa kumlinda kipindi chote cha utumishi wake Jeshini pamoja na maofisa wenzake kwa namna ambavyo alishikiana na kufanya kazi za Jeshi hilo kwa kiwango kikubwa.

Kamishna Dkt Mussa amesema licha ya mafanikio yake ya utumishi ndani ya Jeshi hilo atakumbuka changamoto mbalimbali alizokutana nazo katika utumishi wake ambapo amesema atakumbuka mabadiliko ya tawala ya vyama vingi Zanzibar pia jambo jingine ambalo ni kuzama kwa meli MV Spice iliyotokea miaka kumi na moja iliyopita na kusababisha kupoteza Maisha ya watu wengi Zanzibar.

Pia amewaomba maofisa na askari wa Jeshi hilo kuendelea kushirikiana ili kufanikisha adhima ya Jeshi hilo katika kupambana, kuzuia na kutanzua uhalifu hapa nchini.

Related news