• "NIDHAMU HAKI WELEDI NA UADILIFU, MSINGI WA MAFANIKIO YETU"
Close

DCI afunga mafunzo ya I-EAC jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Camilius Wambura amesema Jeshi la Polisi nchini limejipanga kuhakikisha kuwa hakuna mhalifu anayetamba hapa nchini na wanaofanya uhalifu wataendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria kwakushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (INTERPOL).

DCI Wambura ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa ufungaji wa mafunzo ya mradi wa INTERPOL EAST AFRICA COMMUNITY (I-EAC) kwa Watendaji wa Taasisi mbalimbali  watakaohusika na mradi huo ambao lengo lake ni kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.

Kwa upande wake Mshiriki wa Mafunzo hayo kutoka Wakala wa Usajili ufilisi na udhamini (RITA) ROBBY OTAIGO amesema mafunzo hayo yatawajenga kushirikiana na INTERPOL katika kupambana na uhalifu huku Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Kenya Bi. ALLEN BAMBAZI akisema wanatarajia kuongeza muda wa mafunzo hayo ili kuwafikia watu wengi zaidi.

Related Posts