IGP Simon Sirro akutana na IGP wa Malawi, 10/06/2022 Mbeya Tanzania

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi litaendeleza ushirikiano na Jeshi la Polisi nchini Malawi pamoja na kuendelea kubadilishana taarifa za uhalifu na wahalifu sambamba na kufanya operesheni za pamoja kwa lengo la kuhakikisha nchi hizo zinakuwa salama.

IGP Sirro amesema hayo wakati alipokutana na mgeni wake DR. GEORGE KAINJA ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Malawi ambapo amesema kuwa kutokana na ushirikiano huo kutarahisisha kukamatwa kwa wahalifu wanaofanya uhalifu nchi moja na kuelekea nchi nyingine.

Kuhusus wahamiaji haramu IGP SIRRO amesema, wataendelea kuzishirikisha nchi nyingine katika kukabiliana na changamoto ya uingiaji wa wahamiaji haramu.

Related Posts