UJUMBE WA CPF

Nidhamu haki weledi na uadilifu, msingi wa mafanikio yetu, pamoja na Umoja na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na wananchi ni
silaha kuu itakayotusaidia katika mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu.
Tukishikamana na kuwa na umoja kama wa siafu, hakuna mhalifu
atakayepata nafasi ya kufanya uhalifu popote katika nchi yetu.
Siafu ni wadudu ambao kila mmoja wetu ameshawahi kukutana nao au
kuwafahamu. Hawa ni wadudu wa ajabu sana ambao hutenda kazi zao
kwa umoja na ushirikiano wa hali ya juu huku wakiwa na mgawanyo wa
majukumu kuanzia ulezi wa familia, watendaji kazi mpaka ulinzi wa himaya
zao.
Kutokana na mfumo wao wa maisha utajifunza kuwa duniani silaha kuu
ni umoja na ushirikiano kwani pamoja na udogo wao, siafu wanauwezo
wa kuwapiga na hata wakati mwingine kuwaua adui zao wenye miili na
maumbo makubwa akiwemo nyoka.
Shime wananchi tushikamane na kuungana na Jeshi la Polisi Tanzania
katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu ili Tanzania yetu iendelee kuwa
salama.