Kamisheni ya Zanzibar

Kamisheni ya Polisi Zanzibar ni miongoni mwa kamisheni ndani ya jeshi la Polisi Tanzania, lengo kuu ni kusimamia shughli zote za kipolisi Zanzibar.
Majukumu yake ni:
- Kusimamia masuala yote ya kiutawala, operesheni na upelelezi katika komandi ya Zanzibar
- Kiunganishi katika ya Jeshi la Polisi Zanzibar na idara zote za Serikali na zisizo za kiserikali Zanzibar
- Kubresha maslahi ya wafanyakazi na ustawi wa rasilimali watu katika Kamisheni ya Zanzibar na mikoa yake yote.
- Kufanya kazi nyingine zozote kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi.