Nidhamu Haki Weledi na Uadilifu ni msingi wa mafanikio Yetu.

WhatsApp Image 2024-02-02 at 1.23.15 PM (1)

Kamishna Kaganda asisitiza matumizi ya mifumo

Maofisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali na Watumishi Raia wanaofanya kazi Makao Makuu ya Polisi Dodoma wametakiwa kujifunza na kuelewa vyema Mifumo inayotumika ndani ya Jeshi la Polisi kwa kuwa hivi sasa Jeshi hilo limejikita kuboresha utendaji wake kupitia mifumo.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Polisi, Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu CP Suzan Kaganda wakati akizungumza katika baraza la Askari lililofanyika leo Februari 02 2024 kwa lengo la kutoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha utendaji wa kazi za Polisi Makao Makuu ya Polisi.

Kamishna Kaganda alisema ipo Mifumo mingi ambayo imeanzishwa kwa lengo la kurahisisha utendaji wa kazi ambapo kila Askari na Mtumishi Raia anapaswa kuifahamu vyema kwa
kuwa utumiaji wa karatasi kwa sasa sio kipaumbele tena ndani ya Jeshi la Polisi.

Vilevile amewataka kuwa tayari kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ili uweze kupita salama.
MWISHO

Related news