Kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania

HISTORIA YA JESHI LA POLISI TANZANIA.

Jeshi la Polisi la Tanzania lilianzishwa rasmi 25 August 1919 kwa tangazo la Serikaliya Kiingereza lililotoka Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kwa wakati huo likaitwa Jeshi la Polisi Tanganyika. Lakini jeshi lilianzishwa kisheria kwa Sheria ya uanzishajiwa Jeshi la Polisi ya mwaka 1939 [THE POLICE FORCE AND AUXILIARY SERVICES ACT OF 1939) PRINCIPAL LEGISLATION. Sheria hii ndiyo inatumika hadi sasa japo imekuaikifanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.

Makao Makuu ya Jeshi hilo kulinga na natangazo hilo yalikuwa Wilayani Lushoto Mkoani Tanga chini ya uongozi wa Major S.T Davis.

Baadae Mwaka 1921 Kundi la Wakaguzi Polisi kutoka Ulaya lilifika nchini Tanganyika na kuanzisha Shule ya Mafunzo maalumu ya upolisi huko Mkoani Morogoro ilikukidhi mahitaji yao na kuwana Askari wenye weledi wakutosha. Pamoja na kuwa na Askari weusi waliofunzu mafunzo lakini bado Askari hao walibaki na vyeo vya chini vya Kipolisi kwani vyeo vya juu vyote walipewa AskariWazungu.

Jeshi la Polisi la kikoloni lilikuwa naWanaume pekeyao, hakuna mwanamke aliyepewa nafasi ya kujiungana Jeshi, siyotukwa Watanganyika hata Askari waki koloni wote walikuwa wanaume.
Mafunzo yalilenga kumpa Askari mbinu za kumkandamiza Mwafrika, kuwaminisha kuwa kila walichosema wakoloni ndicho sahihi, ukandamizaji na udhalilishaji kwa Mwafrika ulikuwa mkubwa na ndiyo ilichukua sehemu kubwa ya mafunzo kwa Askari wa Kikoloni. Askar iwalifundishwa utii kwa viongozi wakikoloni na ukatili dhidi ya waafrika hasa viongozi wa kikoloni pamoja na machifu. Lengo lilikuwa ni kumtawala Mtanganyika kirahisi.
Watanganyika alitumia silaha za jadi kukabiliana naAskari wa kikoloni, silaha hizo zilikuwa marungu, panga, mikuki, na mishare, pamoja na silaha zilizotengenezwa kwa mawe yaliyochongwa vyema.

Wakoloni waliona ni vyema waanzishe vituo vingi vya Polisi na mwaka 1925 Kituo cha kwanza rasmi cha Polisi nchini kilifunguliwa huko Lupa, TingatingaMbeya.

Mwaka 1930 MakaoMakuu yaPolisi yalihamishwa kutoka Lushoto Mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam. Lengo lilikuwa kuwa na ngome imara ambayo ilisimamia utendaji wavituo vingin evyote vya Polisi, mawasiliano na maelekezo ya ninikifanyike vituo ni yalitolewa kila siku kwa vituo vyote vya Polisi. Radio na barua za kipolisi zilitumika kufikisha ujumbe vikosini.

Baadaye Mwaka 1949 kikosi cha kutulizaghasia, Motorized Company sasa Field Force Unit (F.F.U) kilianzishwa nchini na lengo la kikosi hicho ni kurejesha amani penye vurugu.
Vijana wa kitanganyika walianza kupinga ukandamizaji wamMkoloni dhidi yao, vijana hao waliongozwa na baadhi ya Askari waliotoka katika vita ya kwanza na ya pili ya Dunia. Hivyo basi iliwalazimu wakoloni kuanzisha kikosi maalum cha kutulizaghasia, pia mwaka huo wa 1949 kwa kuzingatia weredi, Vijana mbalimbali wa Kiafrika tokas hule mbalimbali za Sekondari Tanganyika walichaguliwa kujiungana Jeshi la Polisi na kuwa Wakaguzi wa Polisi chini ya uangalizi wa muda maalum (Probation Inspectors).

Mwaka 1952  Kikosi maalum cha Mawasiliano (Signals Branch) kilianzishwaPolisi bila kutumia nyaya za simu. Lengo la kikosi hicho ni kuhakikisha Jeshi la Polisi lina wasiliana muda wote. Mawasiliano ya lisaidia kutoa na kusamba za taarifa kwa haraka zaidi na utekelezaji wake kufanyika na mwaka huo pia Askari wa kike (Women Police) walijiunga na Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Ms. Payee. Ms. Payee ndiye alikuwa kiongozi wa askari wa kike kwa kipindi hicho.

Mara tu baada ya Tanganyika kupata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961, Jeshi la Polisi lilianza kubadili mwelekeo wake toka katika kutumikia Wakoloni na kuanza kuwatumikia wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali yaWananchi wa Tanganyika japo bado lilikuwa na mfumo wa kikoloni. Ilichukua muda kulibadilisha na kulifanya Jeshi la Polisi liwe la kumlinda Mtanganyika na mali zake.

Wakuu wa Jeshi la Polisi (IGP) toka Tanganyika had isasa.

Toka uhuru mpaka sasa Jeshi la Polisi limeongozwana Ma IGP kumi:-

Camillus M. Wambura (2022-sasa)
Simon N. Sirro (2017-2022)

Ernest J. Mangu (2014-2017)
Saidi A. Mwema. (2006 – 2013)
Omar I. Mahita. (1996 – 2006)
Haroun Mahundi (1984 -1996)
Solomon Lyaani (1980-1984)
Philemon N. Mgaya. (1975 – 1980)
Samweli H. Pundugu. (1973 – 1975)
Hamza Azizi (1970 – 1973)
Elangwa N. Shaidi (1964 – 1970),

Usalama wa Raia na Mali zao

SIMON SIRRO

(2017-2022)
Usalama wa Raia na Mali zao

ERNEST MANGU

(2014- 2017)
Usalama wa Raia na Mali zao

SAID MWEMA

(2006-2013)
Usalama wa Raia na Mali zao

OMAR MAHITA

(1995- 2006)
Usalama wa Raia na Mali zao

HARUN MAHUNDI

(1984-1995)
Usalama wa Raia na Mali zao

SOLOMON LIANI

(1980-1984)
Usalama wa Raia na Mali zao

PHILEMON MUGAYA

(1975- 1980)
Usalama wa Raia na Mali zao

S.H PUNDUGU

(1973 – 1975)
Usalama wa Raia na Mali zao

HAMZA AZIZ

(1972-1973)
Usalama wa Raia na Mali zao

ELANGWA SHAHIDI

(1962-1972)