Nidhamu Haki Weledi na Uadilifu ni msingi wa mafanikio Yetu.

maafisa

Maafisa Polisi Wajengewa Uwezo TPS Moshi

Maafisa Polisi Jamii, Wakaguzi wa Kata/Shehia na Wakufunzi kutoka vyuo vya Polisi nchini, wanaendelea na mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kushirikiana na kufanya kazi na Jamii katika kutekeleza moja jukumu la Jeshi la Polisi la kubaini na kuzuia uhalifu.

Washiriki wa mafunzo hayo ambao idadi yao ni 60 wanatoka katika mikoa ya kipolisi 35 na kutoka katika vyuo vyetu vya Polisi.

Mafunzo hayo yanafanyika katika Chuo cha Polisi Tanzania Moshi Mkoani Kilimanjaro na yanaendeshwa kwa ushirikiano wa maafisa wa Polisi kutoka Royal Thai Police ya Nchini Thailand, Bavarian Police kutoka nchini Ujerumani na Jeshi la Polisi Tanzania.

Mafunzo hayo ya siku nne yalifunguliwa rasmi Juni 19, 2023 na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP, Camillus Wambura.

Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kusikiliza kwa makini, wawe tayari kuwa chachu ya mabadiliko katika kushirikisha na kushirikiana na jamii na kwa kutekeleza mbinu mpya watakazofundishwa katika mafunzo hayo.

Pia Alilishukuru Shirika la Hanns Seidel Foundation kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuzidi kuleta wakufunzi kutoka nchi mbalimbali ili kuwajengea uwezo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Miongoni mwa wakufunzi waliopo katika mafunzo ya awamu hii ni pamoja na Rais mstaafu wa Jeshi la Polisi Jimbo la Bavaria, Bwana Wolfgang Sommer na kutoka Jeshi la Polisi Thailand ni Colonel Jirapong Rujiradumrongcahai, Colonel Seksa Khruakham na Leutnant Colonel Dr, Krisanaphong Poothakool.

Mafunzo haya ni ya awamu ya pili baada yaliyofanyika Machi 13-18 2023 katika chuo hicho ambapo pia washiriki walikua 60 wakiwepo Maafisa wa Polisi Jamii wa Mikoa, Wakagizi wa Kata/Shehia na Wakufunzi kutoka vyuo vya Polisi.

Related news