Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura akikabidhi vyeti vya Pongezi kwa Maafisa na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi ambavyo himaya zao zimefanya vizuri katika kutekeleza Maelekezo ya Makao Makuu ya Polisi yanayotolewa mara kwa mara.
Vyeti hivyo vimetolewa leo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaoendelea Jijini Dar es Salaam.