Nidhamu Haki Weledi na Uadilifu ni msingi wa mafanikio Yetu.

WhatsApp Image 2024-01-31 at 3.45.53 PM (2)

Serikali haina mashaka na Jeshi la Polisi

Serikali ya Mkoa wa Geita yalipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kwa utendaji kazi wake uliotukuka ambao una ufanya Mkoa kuwa salama wakati wote.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Ndugu Martin Shigela amesema kwamba Serikali ya mkoa wa Geita haina mashaka na utendaji kazi wa Polisi kwani wanafanya kazi muda wote usiku na mchana pale huduma yao inapo hitajika ili kuhakikisha usalama unatawala ndani ya mkoa.

Akiongea na maafisa wa Jeshi la Polisi na familia zao pamoja na wananchi waliokusanyika katika viwanja vya Polisi Wilaya ya Geita kwenye sherehe za Siku ya Familia kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita January 28, 2024 amewataka wenza wa askari Polisi kuhakikisha wana wapa ushirikiano wenza wao ili wawe na ustawi mzuri kijamii ili kuwaongezea hamasa kwenye kazi zao.

Vile vile Shigela ameitaka jamii kuwa heshimu askari Polisi kwenye kazi zao kuheshimu miundo mbinu ya Jeshi la Polisi kama vile majengo pamoja na kuwapa ushirikiano hasa kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Safi A. Jongo amewataka askari kuzitunza vizuri familia zao ili ziwe ni sehemu ya faraja kwenye maisha yao.

 

Related news