Kamisheni ya Utawala na Menejimenti ya Raslimali Watu

CP SUZAN KAGANDA
CP SUZAN KAGANDA

Kamisheni ya Utawala na Menejimenti ya Raslimali watu,  ni miongoni mwa kamisheni ndani ya jeshi la Polisi Tanzania, inahusika na kupanga, kushauri na kusimamia masuala yote yanayohusu rasilimali zote ndani ya Jeshi la Polisi.

Majukumu yake ni:

  • Kutoa ushauri kuhusu masuala yote yanayohusu utawala na menejimenti ya rasilimali watu.
  • Kupanga mikakati ya utekelezaji wa masuala ya Utawala na Rasilimali Watu kwa upande wa ajira, upandishwaji vyeo, nidhamu, motisha, utendaji kazi, ustawi wa jamii, maendeleo na mipango ya rasilimali watu.
  • Kuhakikisha kuwa rasilimali watu ndani ya Jeshi la Polisi inafanya kazi kwa weledi na ufanisi ili kufikia malengo.
  • Kuunganisha Jeshi la Polisi na Ofisi ya Raisi na Menejimenti ya Utumishi katika masuala yote ya sheria, sera na utendaji kazi wa watumishi wa umma.